TMDA
Home SPORTS STARS YAANZA KWA SARE YA 1-1 UGENINI.

STARS YAANZA KWA SARE YA 1-1 UGENINI.

DAR ES SALAAM.

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo imecheza mechi ya kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya DR Congo na kufanikiwa kulazimisha sare ya 1-1 kwenye mchezo huo ambao umepigwa kwenye dimba la TP Mazembe nchini Congo.

DR Congo ndo walianza kupata bao kupitia kwa mshumbuliaji wao anayekipiga katika klabu ya Beijing Guoan nchini China Cedric  Bakambu mnamo dakika ya 23 kipindi cha kwanza na baadae Simon Msuva kusawazisha dakika 36 ya mchezo.

Taifa Stars ipo kundi J ikijumuisha timu ya DR Congo, Madagascar na Benin, hivyo mechi ijayo Taifa Stars itacheza na Madagascar kwenye mchezo ambao utapigwa Septemba 7 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea STARS YAANZA KWA SARE YA 1-1 UGENINI.