Home SPORTS SIMBA YAWASHIKURU MASHABIKI WAKE.

SIMBA YAWASHIKURU MASHABIKI WAKE.

 

Mwandishi wetu.

UONGOZI wa Simba umesema Kuwa umefurahishwa na wingi wa mashabiki pamoja na wadau ambao walijitokeza jana Septemba 19 kwenye siku ya tamasha ya Simba Day.

Jana ilikuwa kilele cha maadhimisho ya Tamasha la Simba Day ambalo  lilikuwa limefana na  lilihusisha watu wa aina mbalimbali ambapo mashabiki wengi wa mpira walikuwa wanalifuatilia na wale waliokuwa nje ya nchi.

Barbra Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa amependezwa na mashabiki wa simba walivyojitokeza Kwa wingi katika  tamasha la Simba Day.

“Nimeona nguvu ya mashabiki na timu Yao hivyo sina mengi zaidia ya kufurahishwa n wingi uliojitokeza Jana katika hitimisho la Tamasha la Simba”anasema.

Hata hivyo Katika tamasha Hilo ambapo Simba walikutana  na mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambapo ulipigwa Jana ambapo Simba walipoteza mchezo huo Kwa kichapo  Simba 0-1 TP Mazembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here