Home SPORTS SIMBA YALAMBA MKATABA MNONO

SIMBA YALAMBA MKATABA MNONO

 

Na: Stella Kessy

KLABU ya Simba Leo wameingia  mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya milioni 300 na kampuni ya Emirate ACP itakayokuwa inatoa zawadi kwa mchezaji wao kila mwezi anayechaguliwa na mashabiki wa timu hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema uwepo wa Aluminium katika timu yao unaongeza chachu ya wachezaji kufanya vizuri.

“Tumesaini mkataba wa miaka miwili lengo likiwa ni kuwapa motisha  wachezaji wetu kwa kila mwezi ili waendelee kupambana,” anasema Barbara.

Barbara amesema kampuni hiyo imeamua kuweka pesa baada ya kuona faida ambayo wameipata katika msimu uliopita.

“Awali tulianza kwa kuwaangalia kwa miezi kadhaa, walikuja na kusema wanataka kutoa tuzo kwa ajili ya mchezaji bora wa kila mwezi na baadae kipa na mchezaji bora wa mwaka,” amesema Barbara.

Kwa upande wa  mkurugenzi wa Emirate Aluminium ACP, Deogratius Marandu amesema wameendeleza ndoto yao ya kufanya kazi na Simba.

“Tuna ndoto na Simba na imechangia kuendelea kudhamini tuzo za wachezaji bora wa mwezi kwenye klabu hii,” amesema Marandu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here