Home SPORTS SIMBA YAHAMISHIA HASIRA KWA DODOMA JIJI.

SIMBA YAHAMISHIA HASIRA KWA DODOMA JIJI.

 

Na:Mwandishi wetu.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania  Bara, Simba leo wanaondoka kuelekea Dodoma  kwenye  mchezo unaofuata dhidi ya Dodoma jiji utakaochezwa katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kikosi hicho kitakacho ingia uwanjani kikiwa na hasira baada ya kupoteza michezo moja wa ngao ya jamii pamoja na kutoka sare ya bila kufungana na Biashara United.

kwa upande wa kocha  msaidizi Seleman Matola,  amesema kuwa haikuwa bahati yao kushinda licha ya kupambana kusaka ushindi.

“Haikuwa bahati yetu, wachezaji walipambana kwa namna ambavyo wanaweza lakini tumeshindwa kupata ushindi, matokeo ambayo tunayachukua kuyafanyia kazi mchezo ujao kwani ligi ndio imeanza na huku  kila timu inahitaji ushindi,”.

Kikosi cha simba kitakutana na  Dodoma jiji ambao wametoka kuwachapa Ruvu shooting bao 1-0 katika  Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here