Home SPORTS SIMBA Vs MAZEMBE SIMBA DAY.

SIMBA Vs MAZEMBE SIMBA DAY.

 

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara  Simba wanatarajia  kucheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Mabingwa Afrika TP Mazembe katika  kuadhimisha kilele cha Tamasha la Simba Day Septemba 19  mwaka huu.

Kauli hiyo aliitoa  katika mtandao wa klabu ya Simba,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Barbara Gonzalez amethibitisha kuwa Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo ndiyo wageni waalikwa wa Simba katika mchezo wa Simba Day 2021.

“Nina furaha kuwatangazia Wanasimba na Watanzania wote kwa ujumla kuwa tutacheza na TP Mazembe siku ya Simba Day September 19 mwaka huu 2021″

“Tayari tumekamilisha taratibu zote za kuwaalika na sasa ni rasmi kuwa wao ndiyo watakuwa wageni wetu”, anasema Barbara.

Barbara ameongeza kuwa TP Mazembe ni mojawapo ya timu zenye heshima kubwa Barani Afrika na ni heshima kubwa kwa Simba kupata fursa ya kucheza nayo.

Barbara pia anasema kuwa lilikuwa lengo la uongozi na benchi la ufundi kuhakikisha Simba inapata timu nzuri Ili kujua ni wapi hasa kikosi cha msimu huu kipo kwenye maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Bara Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

TP ndio Mabingwa wa Ligi Kuu nchini DR Congo msimu uliopita wa 2020/2021 ni Mabingwa mara 5 wa CAF Champion League, ni Mabingwa mara 2 wa CAF Confederation Cup, ni Mabingwa mara 1 wa kombe la washindi Afrika na Mabingwa mara 3 wa Super Cup Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here