Home SPORTS SIMBA KUSHUKA DIMBANI KUVAANA NA BIASHARA UTD

SIMBA KUSHUKA DIMBANI KUVAANA NA BIASHARA UTD


Na: Stella kessy.

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Simba leo watachuana vikali na Biashara united  katika michuano ya ligi  msimu wa 2021/22. 

Katika mchezo wa leo simba wanahitaji alama 3 muhimu ili kuweza kurudisha imani kwa mashabiki nakupunguza presha kwa wachezaji wao  baada ya kupoteza mechi ya ngao ya jamii.

Katika kuelekea mchezo wa leo kocha msaidizi Seleman Matola ameweka wazi kuwa utakuwa mgumu kutokana na uimara wa wapinzani wao hasa wanapokuwa nyumbani ingawa wamejipanga kwa hali yoyote.


Hata hivyo kocha huyo amewataka mashabiki wa simba kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa hamasa wachezaji huku akihaidi kupambana hadi mwisho kuhakikisha wanapata tatu za ugenini.

“Maandalizi yapo safi na yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na lengo letu ni moja kushinda Ili kuanza ligi vizuri kikubwa tunawaomba mshabiki wajitokeze kwa wingi”amesema.

Hata hivyo aliongeza kuwa Katika mchezo huo wachezaji ambao wataukosa mchezo ni Sadio Kanoute, Joash Onyango  ambao walipata Majeraha katika mechi ya ngao na Mkude alipata msiba  wa kufiwa na mtoto wake.

Katika mchezo mwingine ambao unakutanisha dodoma jiji dhidi ya Ruvu katika dimba la Jamhuli  dodoma,huku Mbeya City watachuana vikali na Tanzania prison.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here