Home SPORTS SIMBA KUKIPIGA NA GALAXY FC

SIMBA KUKIPIGA NA GALAXY FC

 

Na: Mwandishi wetu, DODOMA.

MABINGWA wa Tanzania, Simba wanatarajia kumenyana na Jwaneng Galaxy FC ya Botswana katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika  mwezi ujao.

Hiyo ni baada ya Jwaneng Galaxy kuitupa nje Diplomates FC du 8ème Arrondissement, maarufu kama DFC8 ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye mechi ya kwanza Jijini Gaborone Septemba 11 kabla ya kuchapwa 1-0 jana Jijini Douala.

Katika mechi ya kwanza nyumbani, mabao ya Jwaneng Galaxy yalifungwa na mshambuliaji Muafrika Kusini, Lucky Nhlanhla Mokoena na kiungo Mnamibia, Wendell Rudath, wakati jana bao pekee la DFC8 lilifungwa na kiungo Delphin Mokonou.

Hata hivyo mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC wataanzia ugenini Oktoba 15 Gaborone kabla ya kumalizia nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Oktoba 22.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here