Home SPORTS SIMBA KUENELEA KUWAWEKA FITI WACHEZAJI WAKE KWA MECHI ZA KIRAFIKI

SIMBA KUENELEA KUWAWEKA FITI WACHEZAJI WAKE KWA MECHI ZA KIRAFIKI

Mwandishi wetu

UONGOZI wa Simba umesema kuwa kucheza mechi  za kirafiki ni kupata utimamu wa mwili pamoja na kujua maendeleo ya wachezaji wake.

Kikosi hicho kinachonolewa na  Kocha Mkuu Didier Gomes ambacho  kimeweka kambi Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 na kinatarajiwa kurudi wiki hii kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mwisho.

Katika kuelekea maadhimisho ya  wiki  ya Simba kwenye tamasha la Simba Day ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.

Pia siku hiyo ya tamasha la Simba ni mchezo wa kirafiki kati ya Simba v TP Mazembe unatarajiwa kufanyika huku utambulisho wa wachezaji pamoja na uzi mpya wa msimu wa 2021/22 utafanyika.

Akizungumza Katika Moja ya kipindi Cha michezo Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema hesabu kubwa za kocha kwenye mechi za kirafiki ni kujenga utimamu wa mwili pamoja na kuona uwezo wa wachezaji wao ambao wapo kambini.

Jana Simba ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Fountain Gate na timu hiyo iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mechi zote ambazo wanacheza za kirafiki ni za ndani na hawaruhusu mashabiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here