Home SPORTS SERIKALI KUINUA MICHEZO KWA WANAWAKE

SERIKALI KUINUA MICHEZO KWA WANAWAKE

 Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

SERIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Hassan Suluhu imelenga kuinua wanawake kwenye sekta ya michezo kwa ujumla.

Kauli  hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Hassan Abbas amesema kuwa Tamasha la Michezo la Wanawake Tanzania Tanzanite Festival wanawake wanatakiwa kuamka na  kupata fursa ya kuiwakilishi nchi Kimataifa.

Amesema anaamini kufanyika kwa kongamano hili kutatoa mwongozo wa nini kifanyike kwenye kumuinua mwanamke kimichezo.

Aliongeza kuwa wanawake wa Tanzania wana thamani kubwa sana duniani na ndio sababu iliyoepelekea Tamasha hili kuitwa Tanzanite.

“Tamasha hili limeitwa Tanzanite kwa sababu wanawake wa Tanzania nyie ni wa thamani kubwa sana duniani, Tanzanite inapatikana katika Nchi pekee ya Tanzania,”amesema.

Aliongeza kuwa  kuna baadhi vyama vya michezo vinasema hawapati wadhamini kwenye michezo yao ila kupitia Kongamano hili watatoka na jibu moja namna ya kufanya ili kuhakikisha michezo ya wakina mama inapata fursa  kwa ukubwa wake.

Pia alifafanua kuwa katika Kongamano hilo kutakuwa na mada mbalimbali zitakazojadiliwa ikiwemo hali ya ushiriki wa wanawake katika michezo, taaluma na maadili ya wanawake katika kushiriki michezo na umuhimu wa vyombo vya habari, Udhamini katika ukuaji wa soko la michezo ya wanawake Nchini.

Kilele cha Tamasha la Tanzanite linatarajia kuhitimishwa  Septemba 18 kwa michezo mbalimbali kuchezwa kama vile Rede, michezo ya jadi, Karate, Kuvuta Kamba, Kukuna nazi, Mpira wa kikapu kwa walemavu, Kuruka Kamba na mingineyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here