Home BUSINESS RC MAKALLA AWAPONGEZA WAMACHINGA KWA KUONYESHA USHIRIKIANO ZOEZI LA KUWAPANGA

RC MAKALLA AWAPONGEZA WAMACHINGA KWA KUONYESHA USHIRIKIANO ZOEZI LA KUWAPANGA


– Asema zoezi la kuwapanga linaenda vizuri na ushirikiano ni mzuri.

– siku 30 ni Za kuonyeshwa mahali pA kufanyia BIASHARA 

– Apongeza Viongozi wa Machinga kwa kuwaratibu vizuri wenzao.

– Asema hakuna Mfanyabiashara atakaekosa eneo la kufanya biashara.

Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepongeza na kuwashukuru Wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Kama Machinga wanaofanya biashara Kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa uamuzi wao wa kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.

RC Makalla amewapongeza Viongozi wa Machinga kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa huo wanaozunguka na kutoa elimu kwa Wafanyabiashara wenzao Jambo lililowezesha kujenga uelewa na kufanya Jambo hilo kuwa na mafanikio mazuri.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Wafanyabiashara kushirikiana na Viongozi wao ili waonyeshwe maeneo sahihi ya kufanya biashara pasipo usumbufu wowote.

Miongoni mwa Wafanyabiashara wanaotakiwa kupangwa ni Wale Waliojenga Vibanda juu ya Mitaro na mifereji, Wanaofanya biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu, wanaofanya biashara Kwenye hifadhi ya Barabara, wanaofanya biashara Kwenye mbele ya Maduka na wanaofanya biashara mbele ya Taasisi za Umma zikiwemo shule.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here