Home LOCAL RC MAKALA MARUFUKU HOSPITALI DAR KUZUIA MAITI

RC MAKALA MARUFUKU HOSPITALI DAR KUZUIA MAITI

 Na: HERI SHAABAN

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala ,amewapa onyo kali WAGANGA Wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaozuia wananchi kuchukua maiti za ndugu zao mara baada kufariki.

Mkuu wa Mkoa Amos Makala aliyasema hayo katika ziara ya kero Wilaya ya Kinondoni leo ambapo  amewagiza Waganga Wakuu wote  waliopo katika Mkoa huo mgonjwa akifariki hospitalini mwili huo uwachiwe mara moja.

Naagiza kwa WAGANGA wakuu wote waliopo Mkoa huu mgonjwa akifariki naomba maiti hiyo iachiwe Familia wakaizike kwanini mnakaidi agizo la Serikali ? ambayo imetolewa na Waziri ” alisema Makala.

Makala alisema agizo la kuziachia maiti sio agizo la SIASA limeanza kufanya kazi mara moja mwananchi atakaye zuiwa maiti yake Dar es Salaam apigiwe simu mara moja ili atoe adhabu kwa Mganga mkuu wa Hospitali hiyo ambayo anapingana na agizo la Serikali katika hospitali hiyo.

Amewataka Waganga wakuu kutekeleza agizo la Serikali sio la siasa kuendelea kukaidi na kuzuia maiti ni kukaidi agizo la Serikali katika Mkoa wake.

Wakati huhuo Mkuu wa Mkoa Amos Makala ,amewagiza WAGANGA wakuu wa Mkoa huo kuakikisha kila hospitali za Mkoa huo zinakuwa na dawa muhimu kwa ajili ya matibabu ya Wazee .

Makala alisema amekuwa akizunguka katika ziara zake amekumbana na kero za Wazee kukosa dawa muhimu  katika vituo vya afya na zahanati  wakiandikiwa  dawa wakanunue nje.

“Naagiza kuanzia sasa  WAGANGA wakuu wote muhakikishe kero za dawa katika vituo vya afya na zahanati mnaziondoa mara moja Wazee wapate matibabu na dawa ” alisema.

Katika hatua nyingine alisema Mafuriko mto msimbazi Jangwani Serikali imepatia ufumbuzi wanajenga daraja la kisasa ambalo itamaliza kero wakati wa Mvua

Kwa upande wake Mbunge wa Kinondoni Tarimba Abas alisema mpaka sasa amefanya ziara Kata nane kutatua kero za wananchi wa Jimbo lake na kuzipatia ufumbuzi.

Mbunge Tarimba alizungumzia wananchi wake wa mto ngombe amesema wote wameshalipwa fidia  katika eneo hilo.

Mbunge Tarimba alisema keo kubwa katika Jimbo hilo matibabu ya Wazee kukosa dawa muhimu vituo vya afya na Hospitalini kuzuia maiti mara baada wagonjwa kufariki.

Akizungumzia Maendeleo ya Jimbo hilo alisema Barabara saba zitajengwa kwa fedha za Serikali  ambazo zitasimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA pamoja na ujenzi wa vituo vya afya.

Mwisho

Previous articleYANGA YATUA NCHINI
Next articleBRELA YAHUDUMIA MAMIA YA WANANCHI MAONESHO YA MADINI GEITA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here