Home LOCAL RC MAKALA AWATAKA VIONGOZI WA WILAYA UBUNGO KUSHUGHULIKIA MATAPELI WA ARDHI

RC MAKALA AWATAKA VIONGOZI WA WILAYA UBUNGO KUSHUGHULIKIA MATAPELI WA ARDHI

 

NA: HERI SHAABAN. 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala , amewataka Watendaji Wilaya ya Ubungo vyombo vya dola kuwashughulikia matapeli wa ardhi kufuatia kuwa kero katika Wilaya hiyo na kurudisha maendeleo nyuma.

Makala alisema ameshangazwa kata ya Kwembe kushamili kwa migogoro hiyo ya ardhi na kupelekea changamoto za wananchi migogoro ya ardhi.

“Ninaagiza vyombo vya dola  ,vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia migogoro ya ardhi Kwembe kula sahani moja na matapeli wa ardhi” alisema Makala.

Mkuu wa mkoa Makala alisema katika ziara hiyo atatembea na Wakuu wa Idara wote wa mkoa Wataalam wa Dawasa,Waandisi ,Tanesco,TARURA na viongozi wa kila Halmashauri kujibu hoja na kero za wananchi ambapo leo ziara hiyo itakuwa Wilaya ya Ilala.

Alisema katika ziara hiyo kero zingine zinatatuliwa hapo hapo zingine anazikabidhi kwa Idara husika ambazo zinahitaji ufatiliaji kwa kina kwa ajili ya utatuzi kwa mujibu wa sheria .

Katika kero hizo ambazo zimesumbua Ubungo katika sekta ya ardhi amekabidhi kwa Wilaya ya Ubungo na Halmashauri kutatua mara moja na kutoa majibu  kabla tatizo alijawa kubwa.

Akielezea kero ya maji Jimbo la Ubungo alisema yatapatika kwa asilimia mia na maji ya takuwa ya kutosha ambapo Serikali imetenga shilingi bilioni 5.4kwa ajili ya ujenzi wa tanki kubwa la Lita milioni sita.

Aliwataka wananchi wa Jimbo la Ubungo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu  ambapo tanki hilo la maji linatarajia kukamilika Juni mwakani.

Makalla alisema kukamilika kwa tanki hilo kutasaidia upatikanaji wa maji Safi na Salama  kwa Wakazi wa Jimbo la Kibamba na maeneo jirani ikiwemo Kwembe, Machimbo, Kibwegere, Msigani, Msakuzi kaskazini, Msumi na Kibamba mji mpya.

Aidha  Makalla alisema Ujenzi huo unaenda sambamba na miradi ya Ujenzi wa visima  ambapo amewaelekeza DAWASA kusimamia Mradi huo ukamilike mapema na kuleta tija kwa Wananchi .

Kwa upande wake Meneja wa DAWASA Mkoa Kinyerezi Mhandisi Burton Mwalupaso alisema Mkoa wa DAWASA Kinyerezi unahudumia Kata za Kinyerezi, Bonyokwa, Ukonga, Gongo la Mboto, Pugu na Kwembe DAWASA KINYEREZI wameandaa Mradi wa Maji kutoka Kwembe Serikali ya mtaa hadi Kifuru, mradi huo  uta tekelezwa Katika Jimbo la Kibamba  Kata ya Kwembe ukihudumia  mitaa ya Kinga’zi A, Kinga’zi B na Hali ya Hewa na hadi Kifuru sehemu ya Jimbo la Segerea.

Mwalupaso alisema Mradi huo  utatekelezwa kuanzia September 2021 na kukamilika December 2021.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here