Home LOCAL RC DAR APIGA MARUFUKU MICHANGO SHULENI

RC DAR APIGA MARUFUKU MICHANGO SHULENI

NA: HERI SHAABAN.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amepiga marufuku michango ya Shuleni bila kibali cha Serikali pamoja na Tuisheni.

Mkuu wa mkoa Makala aliyasema  hayo katika ziara yake Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala   ya kutatua kero za Wananchi .

“Ninaagiza katika mkoa wangu wa Dar es Salaam marufuku michango na tuisheni shuleni bila kibali  tutekeleze mpango wa  Elimu bila malipo bila kuwachanja wananchi fedha  alisema  Makala.

Makala alisema   Waraka wa Serikali Elimu bila malipo hivyo walimu wasiwachangishe pesa za tuisheni Wazazi.

Katika hatua nyingine amepiga marufuku ujenzi holela wa vibanda vya viabashara katika maeneo ya shuleni mkoa wa Dar es Salaam bila kufuata taratibu 

Makala alisema kuna baadhi ya shule zimejenga vibanda bila kufuata taratibu katika mkoa wake ni marufuku kuanzia Leo 

Wakati huo huo ameagiza DAWASA Kuweka kambi Buguruni kwa ajili ya kuzibua Mfumo wa maji taka ambao unachafua mazingira ya wakazi wa Buguruni kila wakati.

“Ninaagiza DAWASA kuweka kambi Kata ya Buguruni kutengeneza miundombinu ya maji taka ambayo ni ya muda mrefu imekuwa kero kwa jamii” alisema.

Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa anatembea na wakuu wa Idara wote na Wataalam wake ,baadhi ya mashauri yanatatuliwa hapo hapo mengine anayaekeleza mahala mamlaka husika .

Kwa upande wake Mhandisi wa DAWASA mkoa wa Kinyerezi Burton Mwalupaso alisema DAWASA jukumu lao kuakikisha linasambaza maji safi na Salama kwa wananchi pia jukumu lao lingine kusimamia    maji taka agizo lililotolewa na Mkuu wa mkoa watatekeleza na kutatua kero hiyo.

Mwiaho.

Previous articleMSANII WA BONGO FLEVA WHOZU AZINDUA WIMBO MAALUM WA SIMBA SC
Next articleBENKI YA EXIM YAZINDUA HUDUMA MPYA YA BIMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here