Home BUSINESS NSSF YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA MADINI GEITA.

NSSF YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA MADINI GEITA.

Na: Mwandishi wetu, GEITA.


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya pili katika kutoa huduma bora kwa wananchi katika Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini aliyofungwa rasmi leo na Waziri wa Fedha na Mipango akimuwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kwenye viwanja vya Bombambili Mjini Geita.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kufunga maonesho hayo Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Bi Lulu Mengele amesema kuwa wao kama wamefurahishwa na hatua hiyo kwa kuweza kupata Tuzo hiyo nakwamba wakati wote wataendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wote.

 
“Leo tuna furaha sana tumekuwa washindi wa pili kwenye maonesho haya hii inatokana na huduma bora tulizokuwa tukizitoa hapa wakati wote tumweza kuwahudumia wananchi wengi na wengine wamepata kadi zao za uwanachama hapa hapa kwakweli tunawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuja kupata huduma” Amesema Lulu.

NSSF walipiga kambi kwenye maonesho hayo ya siku kumi yaliyoanza Septemba 16 na fukunguliwa rasmi na Mheshimwa Wazir Mkuu Kassim Majaliwa Septemba 22, ambapo leo yamefikia kilele chake kwa kufungwa rasmi na waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here