Home SPORTS NAMUNGO YAANZA VYEMA YAICHAPA GEITA.

NAMUNGO YAANZA VYEMA YAICHAPA GEITA.

Na: Mwandishi wetu.

KIKOSI Cha  Namungo FC leo kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika michuano ya  Ligi Kuu ya Tanzania katika mchezo uliopigwa  Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

Mabao ya Namungo FC,  yamefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 13 na Relliant Lusajo dakika ya 81.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wageni wakitangulia kwa bao la beki Mghana, Daniel Amoah dakika ya 49, kabla ya Hance Masoud kuwasawazishia wenyeji dakika ya 90.

Na wageni wengine, Mbeya Kwanza wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar bao pekee la William Edgar dakika ya 50 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here