Home SPORTS MO AJIUZULU SIMBA.

MO AJIUZULU SIMBA.

 

Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ametangaza kujiuzulu katika nafasi hiyo baada ya mkutano wa September 21.

Akizungumza katika video ambayo ametupia katika ukurasa wake wa Instagram na facebook Mo ameweka wazi kuwa kwa sasa atabaki kuwa Mwanahisa ndani ya timu hiyo baada ya kukubaliana na Bodi kwamba anajiweka pembeni kwenye nafasi hiyo.

Mo amesema kuwa sababu kubwa ambayo imemfanya akajiengua ni kutokuwa na muda kwa kuwa amekuwa akisafiri mara kwa mara hivyo nafasi hiyo itakuwa mikononi mwa Salim Abdalah, ‘Tryagain’.

Mo amebainisha pia mafanikio ambayo wameyapata kwa muda wa miaka minne ikiwa ni ile ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne pamoja na kuweza kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku akisistiza kwamba bado anaipenda Simba na yupo Simba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here