Home LOCAL MBUNGE KAMONGA ATINGA USIKU KUKAGUA MGODI MKUBWA WA MAKAA YA MAWE ULIOGUNDULIWA...

MBUNGE KAMONGA ATINGA USIKU KUKAGUA MGODI MKUBWA WA MAKAA YA MAWE ULIOGUNDULIWA LUDEWA

Kamonga akionesha  moja ya vipande vya mkaa huo.

Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga akiwa na Vincent Malima Meneja Mwendeshaji wa Mgodi mpya mkubwa wa Makaa ya Mawe  uliogunduliwa katika Kitongoji cha Ndambasi, Kijiji cha Masimavalafu,Kata ya Ibumi, wilayani Ludewa, Njombe. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya wazawa ya Maximum Group of Companies  utakuwa unazalisha tani 100,000 kwa mwezi. Kulia ni Mtaalamu wa miamba,  Gerald Buluma.

Akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo

Kamonga akiangalia makaa ya mawe ambayo tayari yameshachimbwa katika mgodi huo.

Ripoti ya Richard Mwaikenda,(CCM Blog) LUDEWA.

MBUNGE wa Ludewa ametembelea usiku Mgodi mpya mkubwa  wa makaa ya mawe uliogunduliwa katika eneo la Kitongoji cha Ndambasi, Kijiji cha Masimavalafu, Kata ya Ibumi, wilayani Ludewa, Njombe kujionea jinsi unavyofanya kazi.


Kilomita moja kabla ya kuingia eneo la mgodi, karibu na Mto Liugai, Kamonga  alikuta lundo la makaa ya mawe zaidi ya tani 700  hali ambayo ilimpa matumaini kuwa kweli kuna  uchimbaji wa madini hayo. ((PICHA ZOTE, NA: RICHARD MWAIKENDA).



Eneo la Mgodi huo wa makaa ya mawe.

Alipofika eneo la mradi huo alikaribishwa na Meneja Mwendeshaji wa mgodi huo, Vincent Malima na hatimaye kutambulishwa  kwa wafanyakazi takribani 20 ambao aliambiwa asilimia kubwa wameajiriwa kutoka vijiji jirani na mgodi huo.

Malima alieleza kuwa kampuni tayari imeshapata kibali  cha kuendesha mradi huo na kwamba wakishaingiza mitambo ya kisasa watakuwa wanachimba takribani tani 100,000 kwa mwezi ambazo tayari zimepata wateja.


“Tupo tayari kulipa kodi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na Serikali Kuu,”amesema Malima.


Ili kurahisisha uendeshaji wa mradi huo mkubwa, Malima ameiomba Serikali kujenga miundombinu ya barabara na umeme kwenda kwenye mgodi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here