Home SPORTS MAYELE APELEKA USHINDI JANGWANI.

MAYELE APELEKA USHINDI JANGWANI.

Na: Stella Kessy , DAR ES SALAAM.
MSHAMBULIAJI  Mkongo, Fiston Kalala Mayele aipatia Yanga bao la ushindi  ambalo imeipa  Yanga SC ushindi wa 1-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii jioni hii Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salam.

Mayele aliyesajiliwa msimu huu kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa alifunga bao hilo dakika ya 11 akimalizia pasi nzuri ya kiungo mzawa, Farid Mussa Malik.

Simba SC, washindi wa Ngao kwa misimu minne mfululizo iliyopita walimaliza pungufu baada ya kiungo wao Mganda, Thadeo Lwanga kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu kiungo Mzanzibari wa Yanga, Feisal Salum.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here