Home SPORTS MASHABIKI YANGA RUKSA MECHI DHIDI YA RIVERS UTD

MASHABIKI YANGA RUKSA MECHI DHIDI YA RIVERS UTD

Mwandishi wetu.

KLABU ya Yanga SC imeruhusiwa kuingiza mashabiki katika mchezo wake dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Kikosi cha Yanga kitakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaochezwa majira ya Saa 11:00 jioni siku ya jumapili katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo  timu hizo zinatarajia kurudiana Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.

Huku vimetajwa viingilio  vya mechi hiyo ambavyo ni Sh. 30,000 VIP A, 20,000 VIP B, 10,000 VIP C na 5,000 kwa mzunguko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here