Home LOCAL MARAGASHIMBA AWAWEZESHA SAUTI YA JAMII KIPUNGUNI

MARAGASHIMBA AWAWEZESHA SAUTI YA JAMII KIPUNGUNI

NA: HERI SHAABAN.

MWENYEKITI wa Serikali  ya Mitaa Kipunguni Daniel Malagashimba amesema atalipia gharama za usajili Tovuti  Taasisi ya SAUTI YA JAMII KIPUNGUNI ili waweze kutuma taarifa za taasisi hiyo.

Malagashimba alisema hayo Dar es Salaam leo,wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo iliyopo Kipunguni Wilayani Ilala.

“Ofisi yangu ya Serikali za Mitaa Kipunguni nimejenga kwa gharama zangu kwa ajili ya kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kuzinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ili wananchi wapate huduma bora.

Malagashimba alisema katika kuisaidia Serikali na Vikundi vya Jamii amesema atalipia gharama za usajili (Tovuti ya Sauti ya Jamii ili wawe wanarusha Taarifa zao za Kijamii na kuitangaza Kipunguni pia kupitia Mfumo wa TEHAMA.

Malagashimba    alitaka vituo vingine kuiga mfano wa  Taasisi ya Sauti ya Jamii Kipunguni ambayo inatoa elimu na kuisaidia Serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa SAUTI YA JAMII Kipunguni Selemani Bishagazj alisema Sauti ya Jamii imeanza 2014  inashughulika na masuala mbalimbali yakiwemo ya ukeketaji sambamba na kutoa elimu kwa Jamii.

Bishangazi alisema SAUTI YA JAMII KIPUNGUNI kwa sasa ina miliki mradi wa Genereta ,Viti, Mziki, Mahema ya kukodisha vyote sehemu ya Miradi yao chanzo cha Mapato .

Akielezea mikakati ya taasisi hiyo kufungua Mfuko wa ukatili kwa ajili ya kuisaidia Jamii katika Kata sita ambazo  wanatoa huduma zao ndani ya Wilaya Ilala.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Lilian Liundi alisema Bishagazi ni mtu muhimu kwa Jamii Serikali imtumie katika mambo mbalimbali yanayohusu Jamii .


Lilian aliwataka wananchi wa Kipunguni na Sauti ya Jamii wawe Wabunifu na kubuni miradi ya kuwawezesha kiuchumi ili waweze kujikwamua kiuchumi wapate kipato.

Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania imewawezesha wananchi wake kiuchumi kupitia Rais wetu Samia Hassan Suluhu fursa zipo wazi na sasa ametaka majukwaa ya kiuchumi yote yaanzishwe kwa ajili ya fursa.


Alisema Kata ya Sauti ya Jamii inatekeleza Ilani ya CCM hivyo inatakiwa kuungwa mkono ili waweze kuisaidia Jamii na kufikia malengo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Bonyokwa SHAABAN MARYATABU aliomba ifunguliwe Taasisi ya Sauti ya Jamii Bonyokwa iwe inashughulikia wananchi wa Mtaa huo.

Mwisho



LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here