Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem Ikulu Chamwino mkoani Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao yaliofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amemuhakikishia Dkt. Ghanem kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika masuala mbalimbali ya kuinua uchumi hapa mnchini.
Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema kwamba serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika kuinua sekta binafsi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hapa nchini. Amesema mpango wa maendeleo wa miaka mitano umelenga kuinua sekta ya viwanda hapa nchini hivyo serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kufanikisha hilo.
Aidha Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema ili kukidhi mahitaji ya sekta binafsi hapa nchini serikali imeweka mkazo katika sekta ya elimu hasa elimu ya ufundi ili kupata wahitimu wenye ujuzi watakaoweza kusaidia kuinua sekta hiyo.
Makamu wa Rais amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuimarisha utawala bora pamoja na kudhibiti rushwa hapa nchini hivyo kuweka mazingira rafiki ya kutekeleza miradi mbalimbali.
Kwa upande wake makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem ametaja maeneo ambayo benki hiyo itashirikiana na Tanzania ambayo ni pamoja na uboreshaji miundombinu, , mapambano dhidi ya uviko19 pamoja na kuinua uchumi baada ya janga la Uviko 19.