Home LOCAL MAJALIWA ASHIRIKI KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA KIGOMA

MAJALIWA ASHIRIKI KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA KIGOMA

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa akiwa ameweka simu kwenye kinasa sauti kuwawezesha washiriki wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma kumsikia Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ambaye alizungumza na wajumbe hao kwa njia ya simu wakati kikao hicho kikiendelea kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, Septemba 16, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa akizungumza wakati aliposhiriki katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, Septemba 16, 2021. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba na kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mkoa wa Kigoma, Abdulkadir Mushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma wakimsikiliza, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashuri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, Septemba 16, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya CCM, Edibily Kinyoma ambaye amekihama cha ACT Wazalendo na kujiunga na CCM katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, Septemba 16, 2021. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba na wa tatu kulia ni Katibu wa CCM wa Mkoa Kigoma, Kajoro Vyohoroka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here