Home SPORTS MAJALIWA AONGOZA MBIO ZA HISANI ZA BENKI YA NMB

MAJALIWA AONGOZA MBIO ZA HISANI ZA BENKI YA NMB


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mazoezi ya viungo baada ya kumalizi mbio za Hisani Benki ya NMB (NMB Marathon 21) zilizoanzia kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam kupitia Oysterbay na kuishia kwenye viwanja hivyo, Septemba 25, 2021. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala, wa pili. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhende na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kumaliza mbio za kilomita 5 zilizoanzia Viwanja via Leaders kupitia Oysterbay na baadae kurejea Leaders Club kijijini Dar es salaam,



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivishwa medali ya ushindi wa mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon 2021) na Mwenyekiti wa Benki hiyo, Dkt. Edwin Mhende baada ya kumaliza mbio hizo zilizoanzia Viwanja vya Leaders Club kupitia Oysterbay na kuishia kwenye viwanja hivyo jijijini Dar es salaam.
 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi milioni 400, 000,000/= , Afisa Mtendaji Mkuu wa CCNRT, Brenda Msangi (aliyenyosaha mkono) baaada kumalizika kwa mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon 21) zilizoanzia kwenye viwanda vya Leaders Club kupitia Oysterbay jijini Der es salaam, Septemba 25, 2021. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Mwenyekti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB, Dkt.. Edwin Mhenda na Kulia ni Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here