Home LOCAL LHRC YAOMBA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MAKOSA YA JINAI.

LHRC YAOMBA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MAKOSA YA JINAI.

 

Na: Farida Saidy,Morogoro

Kituo cha sheria na haki za binaadamu nchini Tanzania kimesema sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ambayo imefanyiwa marekebisho Mwaka 1985 kwa kuondoa kifungu kinachoipa mahakama kuu kutimiza maombi ya dhamana hata katika makosa yasiokuwa na dhamana imepelekea mtuhumiwa kupewa dhamana kama anapewa zawadi badala ya haki.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Kituo cha sheria na haki za binaadamu nchini Tanzania Wakili Ana Henga, Mjini Morogoro Septemba 6, 2021 wakati akifungua kikao kazi cha wadau kwaajili ya kutoa wasilisho la ripoti ya makosa yasiyo na dhamana.

Credit – Fullshangwe Blog.

Wakili Ana Henga amesema ni wakati muafaka wa nchi ya Tanzania kuweka maboresho ya mfumo wa dhamana kutokana na mfumo uliopo sasa kuminya haki za Binaadamu na kumuumiza mtu kimwili na kisaikologia.

Aliongeza kuwa kituo cha sheria na haki za binaadamu (LHRC) kiliangalia mfumo wa utoaji haki ya dhamana hapa nchini kwa kipindi cha mwaka 1945 hadi 2021 kuwa sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1945,ambapo iliipa mamlaka mahakama kuu kusikiliza maombi ya dhamana hata katika makosa yasiyo na dhamana.

”sheria hii ilidhihirisha kwa vitendo dhamana ya uhuru pamoja na dhana yakutokuwa na hatia hadi pale mahakama itakapothibitisha hivyo katika kipindi cha kuanzia mwaka 1945 hadi 1984 mahakama kuu ilikuwa na uwezo huo katika makosa yasiyo na dhamana , kwa bahati mbaya sheria na mwenendo wa makosa ya jinai 1985 iliondoa kifungu kilichoipa mahakama mamlaka hiyo hivyo kwa sasa mtu atakaye tuhumiwa na kosa lisilo na dhamana uhuru wake unapokonywa mpaka kesi yake itakapo hitimishwa na mahakama”.Amesema Wakili Henga

Aidha alisema utafiti huo uliofanywa na LHRC ulifanya ulinganifu wa mfumo wa utoaji haki katika nchi tano (5) za kenya , uganda, malawi , zambia na Zanzibar.

“Niseme tu kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka katika mifumo ya nchi za jirani ili kuboresha mfumo wetu na ni imani yetu kwamba mkutano huu utachochea mabadiliko na hoja zenye uzito baada ya kupata mwanga wa kufahamu kwa kina kutoka wasilisho la leo.” Amesema Ana Henga.

Henga ameongeza kuwa mchakato wa upatikanaji haki kupitia mfumo uliopo sasa wa haki ya jinai unapingana na dhana iliyopo nchini ya ibara ya 13 (6)b ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayoweka dhana ya msingi ya kutokuwa na hatia hadi mahakama itakapothibitisha.

Previous articleRAIS MH.SAMIA SULUHU ASALIMIANA NA ANANCHI WA KARATU
Next articleSTARS KUUNGURUMA TENA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here