Home SPORTS KMC YAJIPANGA KUICHAPA COASTAL UNION

KMC YAJIPANGA KUICHAPA COASTAL UNION

Na: Stella kessy


UONGOZI wa  KMC umesema kuwa licha ya kupoteza mchezo wao wa kwanxa dhidi ya Polisi Tanzania  sasa wamejipanga kufanya vyema dhidi ya Coastal Union  dimba la nguvu zake zote karatu.

Kikosi cha KMC kilipoteza mchezo wake wa kwanza  dhidi ya  Polisi Tanzania 2-0 KMC jambo lililowafanya wapoteze furaha kwa kuziacha pointi tatu mazima.

Akizungumza na mwandishi wa blog hii Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania hivyo nguvu zao wanazipeleka kwenye mchezo ujao.

Itakuwa ni Oktoba 2, pale Uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wao wa ufunguzi.

Ikumbukwe kwamba kabla ya mchezo wa KMC kukamilika kuchezwa Uwanja wa Karatu ulibadilishwa viwanja mara mbili ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika kisha ukapelekwa Uwanja wa Sheik Amri Abeid kisha ukaibukia Karatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here