Home BUSINESS KAMPUNI YA SGA YAZIDI KUJIIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA BORA

KAMPUNI YA SGA YAZIDI KUJIIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA BORA

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Kampuni ya SGA Bi. Faustina Shoo (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Madini Dkt. Dotto Bitteko (kushoto) mara baada ya kutembelea banda la SGA na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo kwenye Maonesho ya Madini Mjiini Geita.
 

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Kampuni ya SGA Bi. Faustina Shoo (kulia) akimkabidhi zawadi kwa Mbunge wa Geita Msukuma Kasheku (kushoto) walipomaliza ziara ya kutembelea mabanda kwenye maonesho hayo.


Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa kampuni ya SGA Bi. Faustina Shoo (kulia) akimkabidhi zawadi Mbunge wa Bukombe kwenye maonesho hayo Mjini Geita.


Ofisa Masoko wa SGA Flora Phanuel (kushoto) akizungumza na mwananchi aliyetembelea kwenye Banda lao kutaka kupata elimu namna kampuni hiyo inavyofanya shughuli zake.

Meneja Msaidizi kitengo cha mifumo ya Teknolojia Mhandisi Godfrey Luture akielezea namna vifaa vya Kielektroniki vinavyofanya kazi katika sekta ya ulinzi. (katikati) ni Ofisa Masoko wa SGA Flora Phanuel, na (wa kwanza kushoto) ni Mteja aliyetembelea Banda lao.

Na: Mwandishi wetu.

Sekta ya ulinzi katika jamii ni kitu muhimu sana hasa kwenye maeneo ya kazi ambapo kila mtu anahitaji kuwa na uwakika wa usalama mahala anapofanyia kazi ama anapoishi.

Hii imepelekea wadau kwenye sekta hiyo kuongeza jitihada za kuhakikisha muda wote kunakuwa na usalama mahala pa kazi ama kwenye makazi yao kwa kwa kutumia Teknolojia mbalimbali za kisasa katka kuhimarisha sekta ya ulinzi .

Kampuni ya ulinzi ya SGA Security ni kampuni kongwe na pekee Tanzania iliyojikita katika suala zima la ulinzi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo katika Migodi, Taasisi Binafsi na za Serikali, Mashirika ya Kimataifa na Balozi mbalimbali na watu binafsi.

Aidha SGA ni Kampuni pekee ya ulinzi Tanzania iliyothibitishwa kwa ubora WA viwango vya Kimataifa kutoa huduma bora na za viwango vya juu na kupewa vyeti vya ubora vya Kimataifa kiwemo ISO 9001:2018 (QMS), 1SO 45001:2018 (QH&S), na ISO18788:2015 Security Operations Management System (SOMS).

Bi. Faustina Shoo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Kampuni ya SGA anasema kuwa Kampuni yao inatumia Teknolojia ya kisasa katika kufanya shughuli zake za ulinzi lengo likiwa ni kuhakikisha kunakuwepo usalama wa kutosha kwa mteja na watu wote kwa ujumla.

“Kampuni imeweza kufanya shughuli zake kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia Teknolojia ya kisasa na watalaamu waliobobea kwenye Teknolojia hizo ndio maana tumewza kupata tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya utoaji wa huduma bora kwa wateja wetu ya mwaka 2020 na kutoka ajira kwa zaidi ya Watanzania 6,000” amesema Bi. Faustina.

Pia amezungumzia ushiriki wao kwenye Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea kwenye uwanja wa Bombambili Mjini Geita ambapo kampuni ya SGA ni sehemu ya wadhamni waliojitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua sekta ya madini nchini na wadau  wote wanaojihusisha kwenye Sekta hiyo.

“Sisi kwenye Maonesho haya ni sehemu ya wadhamini lakini pia sekta ya madini imekuwa na changamoto kwenye masuala ya ulinzi hivyo Kampuni hii imekuwa ikitoa huduma za ulinzi wa watu, na kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mitambo ya kisasa inayotumia Teknolojia ya kisasa katika usalama wa watu na mali zao kwenye maeneo ya migodini na maeneo mengine” Ameongeza Bi. Faustina.

Maonesho  hayo ya Teknolojia ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ni maonesho ya Nne kufanyika Mkoani Geita yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza Teknolojia za kisasa katika sekta hiyo ikiwemo kutoa elimu kwa wadau kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ulinzi kwenye migodini.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here