Na: Mwandishi wetu.
MAHAKAMA ya Usuluhishi ya Shirikisho la soka Duniani (CAS) wameahirisha kutoa uamuzi wa kesi ya Yanga na Bernard Morrison kutoka leo Septemba 21 hadi Oktoba 26 mwaka huu.
Mmoja ya Mawakili anayewakilisha Yanga katika kesi hiyo Alex Mgongolwa amesema amepokea taarifa ya CAS leo ikieleza sasa hukumu hiyo imesogezwa mbele mpaka Oktoba 26.
“Siku zote ukiona kama hukumu inasogezwa mbele basi mleta shauri ana hoja ndio maana unaona hivyo, kwa hiyo tunasubiri maamuzi hayo,” .
Suala kubwa kuhusu kesi ya Morrison ni ishu ya mkataba wake ambapo aliweza kusaini mkataba Simba huku Yanga wakidai kwamba bado alikuwa ni mali yao.
Kwa upande wa mchezaji mwenyewe, Morrison amekuwa akieleza kuwa alisaini dili la miezi sita na ilipoyeyuka hakusaini dili jingine.
Hivyo kwa sasa ni suala la majibu ambayo yanatarajiwa kutolewa Oktoba 26 ili kujua majibu kutoka CAS.