HOSPITALI ya Harmony Memorial Polyclinic kufungua chuo cha Manesi Kata ya Bonyokwa Wilayani Ilala
Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Hospitali ya kisasa Harmony Memorial Polyclinic Julian Mmari wakati wa uzinduzi wa Hospitali hiyo iliyozinduliwa na Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli.
Mkurugenzi Mmari alisema mikakati ya Hospitali ya Harmony Memorial Polyclinic inatarajia kujenga chuo cha HARMONY Kata ya Bonyokwa ili kiweze kuzalisha manesi wa kisasa waweze kuisaidia Serikali katika kada ya sekta ya afya.
Mmari alisema wakati wanamia Bonyokwa huduma za zahanati ni shida mama wanasafiri umbali mrefu kutafuta Kituo cha afya ndio wakapata ndoto ya kujenga Kituo hicho kikubwa chenye madaktari Bingwa ambacho kinatoa huduma zote za afya zikiwemo za mama na Mtoto .
Mmari alisema Kituo chao cha afya taratibu za usajili wameanza mwezi Mei kimesajiliwa kina watumishi 21 kwa sasa.
Akielezea Changamoto alisema changamoto kubwa miundombinu ya Barabara ni mbovu kufika Harmony Hospitali tunaomba Mbunge Bonah na Serikali itusaidie .
Kwa upande wake mgeni rasmi Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli alimpongeza Mkurugenzi wa Hospitali ya HARMONY kujenga Kituo cha afya kikubwa Bonyokwa.
Mbunge Bonah alisema Bonyokwa imezaliwa kutoka kata ya Kinyelezi ili kuwa kubwa ikagawanywa ikazaliwa Bonyokwa , Jimbo linatakiwa kuwa na vituo vingi vya afya ili waweze kutoa huduma za afya karibu na wananchi.
Akielezea miundumbinu ya Barabara alisema baadhi ya Barabara zipo chini ya TANRODS na zingine zipo katika usimamizi wa TARURA
Bonah alisema kuhusu kero ya kipande cha Barabara mpaka kufika Hospitalini hapo amelichukua ataitatua kwa haraka ili wagonjwa wakiingia na magari wasipate kero yoyote.
MWISHO