Home BUSINESS HABARI PICHA: WATUMISHI WA WIZARA YA MADINI IKIZUNGUMZA NA MKUU WA MKOA...

HABARI PICHA: WATUMISHI WA WIZARA YA MADINI IKIZUNGUMZA NA MKUU WA MKOA WA GEITA KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA


Mwanasheria wa Wizara ya Madini Godfrey Nyakisinda (wa kwanza kushoto) akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule (kulia) wakati wa ziara ya viongozi kutembelea mabanda katika maonesho ya Madini Mjini Geita. (wa pili kushoto) ni Kaimu Kamishna wa uongezaji thamani kutoka Wizara ya Madini Betha Luzabiko.


Kaimu Kamishna wa uongezaji thamani kutoka Wizara ya Madini Betha Luzabiko. (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amina Makiragi (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule (wa pili kulia) walipokuwa kwenye Banda la Wizara ya madini kupata maelezo kutoka kwa mtaalamu huyo kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta hiyo kufuatia marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2010 yaliyofanyika mwaka 2017.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita Zahara Michuzi wakiongozana kuelekea kwenye Banda la wizara ya Madini kuanza ziara ya kukagua Mabanda kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Sekta ya Madini yanayoendelea kwenya uwanja wa Bombambili Mjini Geita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here