Home LOCAL DKT. KALEMANI: WAKANDARASI WASIONDOKE ENEO LA MRADI KABLA YA KUKAMILISHA KAZI

DKT. KALEMANI: WAKANDARASI WASIONDOKE ENEO LA MRADI KABLA YA KUKAMILISHA KAZI

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Nhinhi, wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, alipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho, Septemba 3, 2021.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(kushoto), akikabidhi kifaa cha Umeme Tayari( UMETA), kwa wakazi wa Kijiji cha Nhinhi, wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, alipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho, Septemba 3, 2021.

Mbunge wa Jimbo la Mvumi, Livingston Lusinde (kulia) akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Nhinhi, wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, wakati Waziri wa Nishati, Dkt. Medard(wa pili kulia waliokaa) Kalemani alipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho, Septemba 3, 2021.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(katikati) akikata utepe pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali, alipoakizungumza na wakazi wa kijiji cha Nhinhi, wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, alipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho, Septemba 3, 2021, wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Gift Msuya.

Na: Zuena Msuya, DODOMA.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeza Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA), kuwepo maeneo ya mradi wakati wote wa utekelezaji wa mradi huo hadi pale watakapokamisha kazi hiyo.

Dkt.Kalemani alisema hayo wakati akiwasha umeme katika soko la Kijiji cha Nhinhi wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Septemba 3, 2021.

Alifafanua kuwa kumekuwa na baadhi ya wakandarasi kutokuwepo katika maeneo ya mradi na hivo kusababisha utekelezaji wa mradi hiyo kutokwenda kwakasi inayotakiwa.

“Mkandarasi wote wanaotekeleza mradi wa usambazaji wa umeme hapa nchini mnatakiwa kuwepo maeneo ya mradi hii inafanya kazi zinaenda haraka na kwa usahihi mkubwa, nikimtambulisha mkandarasi kwa wananchi anatakiwa abaki eneo la mradi na afanye kazi kwelikweli tunataka mradi huu ukamilike hata kabla ya muda uliopangwa lakini kwa ubora unaotakiwa” alisema Dkt. Kalemani.

Aidha aliweka wazi kuwa mradi huo wa usambazaji wa umeme vijijini Awamu ya Tatu Mzungunguko wa Pili utakamilika ndani ya kipindi cha miezi 18, kwa kwamba serikali haitaogeza muda kwa yeyote atakayechelesha mradi huo.

Alirejea kueleza kuwa mkarandarasi atakaechelewesha mradi ndani ya kipindi kilichoelezwa katika mkataba wa Makubaliano atakatwa asilimia kumi (10%) ya malipo yake.

Alisema kuwa Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa vijiji na vitongoji vyote nchini vinapata umeme kabla ya Desemba 2022, hivyo haitavumilia kuona mtu yeyote anaonyesha dalili za kuuchelesha.

Katika Hatua nyingine aliwataka wananchi wa eneo hilo kutandaza nyaya katika nyumba zao na kulipia gharama ya shilingi 27,000 tu pasipo kulipishwa gharama za nguzo, nyaya pamoja na mita ili waunganishiwe umeme.

Vilevile aliwataka wananchi hao kulinda miundombinu ya umeme na pia kutoa taarifa katika ofisi za Serikali za Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa pamoja na TANESCO, pale watakapoona ama kubaini mtu yeyote anahujumu miundombinu hiyo ili achukuliwe hatua za kisheria.

Aidha aliwataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo na kuchangamkia fursa ya kufanya kazi zisizohitaji taaluma maalum, ili waweze kujiongezea kipato na kufurahia uwepo wa mradi huo katika maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here