Home LOCAL DIWANI NYASIKA AWATAKA WANANCHI KIVULE KUSHIRIKI SENSA KWA MAENDELEO

DIWANI NYASIKA AWATAKA WANANCHI KIVULE KUSHIRIKI SENSA KWA MAENDELEO

Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama (katikati)akikabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani 2021 leo September 17/2021 kwa Mwenyekiti wa CCM kata Kivule Hemed Nyangum (PICHA NA HERI SHAABAN).

DIWANI wa Kata ya Kivule Nyasika Getama akiongea na Waandishi wa Habari Dar es Salam Jana wakati wa kuwasilisha Taarifa za utekelezaji wa Ilani (PICHA NA Heri Shaaban).

NA HERI SHAABAN( ILALA)

DIWANI wa Kata ya Kivule Nyasika Getama amewataka wakazi wa Kivule kushiriki SENSA ya Makazi kwa ajili ya kuhesabiwa ili waweze kuletewa Maendeleo ndani ya Kata Kivule.

DIWANI Nyasika alisema hayo wakati wa kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Desemba 2020 mpaka Agosti 2021.

Diwani Nyasika alisema Serikali  inatarajia kufanya sensa ya Makazi mwakani  2022 kwa Wananchi wake hivyo wananchi wa Kata Kivule wote watumie fursa hiyo wahesabiwe watambulike waweze kuletewa Maendeleo.

“Maendeleo ni muhimu kwa nchi yoyote nawaomba Wajumbe wa mashina Wenyeviti wa Serikali za mitaa wote mtoe elimu katika kuwaeleza umuhimu wa SENSA wananchi wetu Kivule ilizaa Kata ya Kipunguni awali na sasa Idadi ya wananchi wameongezeka hapa Kivule hivyo lazima tuwatambue” alisema Nyasika

Alisema SENSA wakati ukifika kila MTU lazima awepo itamtamburisha yupo wapi kutokana na Giografia ya Kata yetu kwa sasa kutokana na Changamoto za Mipaka eneo la Magole  na Vikao vya Ushauri ngazi ya Wilaya ILALA RCC vitatoa maamuzi yake .

Akizungumzia Maendeleo ya Kata Kivule alisema sekta ya Elimu kuna shule za msingi mbili za sekondari nne amejenga madarasa mawili  kwa upande wa shule za msingi sekondari amejenga madarasa kumi na kununua madawati 58 .

Mikakati yake katika utekelezaji wa Ilani ya CCM 2122 kuongeza kidato cha kwanza mpaka kidato cha sitq katika shule za Ally Jumaa na Misitu ili watoto wasome karibu na Kata yao kuwaondolea usumbufu awali ili kuwa mwisho kidato cha NNE.

Mikakati yake mingine kwa mwaka 2122 Kuboresha Barabara na kuanzisha safari za ruti ya Daladala mpaka mjini kwa ajili ya kuwaondolea kero Wananchi.

Akielezea changamoto kubwa iliyopo Magole ukosefu wa shule inapelekea wananchi wake kupata shida ya Wanafunzi kwenda umbali mrefu kutokana na Giografia ya Mipaka na mgogoro wa Kivule na   Msongola.

Aliwagiza Wajumbe wa Mashina kuwaorodhesha wananchi wake waliopo katika kaya masikini ili waweze kupitiwa na mradi wa Serikali wa TASAF wasiweke watu wenye sifa katika mradi huo wakaacha watu wenye Vigezo.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Kata hiyo Isac Kibiti aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kumaliza changamoto zao na kuisaidia Serikali katika kuleta Maendeleo ikiwemo kusimamia miradi ya Maendeleo na Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here