Home LOCAL DIWANI LUCY KAMATI YA SIASA WAKAGUA MIRADI KISUKURU

DIWANI LUCY KAMATI YA SIASA WAKAGUA MIRADI KISUKURU


NA: HERI SHAABAN (ILALA).

DIWANI  wa Kata Kisukuru Lucy Lugome na  wajumbe na Wajumbe wake wa Kamati ya Siasa  Kata ya Kisukuru leo wamefanya ziara katika Kata hiyo kuangalia miradi ya Maendeleo ,ambapo Kamati ya Siasa walimpongeza Diwani Lucy kwa utekekezaji wa Miradi ya Maendeleo.

Akizungumza katika ziara hiyo Diwani Lucy Lugome alisema anapata ushirikiano katika chama na Serikali katika usimamizi wa miradi yote ya Kata hiyo.

“Leo nimefanya ziara ya Kamati ya Siasa ya Kata yangu kuangalia utekelezaji wa  Ilani na Maendeleo ambayo nimefanya ndani ya Kata hii kwa ushirikiano na chama na Serikali ” alisema Lucy .

DIWANI Lucy alisema tumekagua Kituo cha Polisi kuangalia Maendeleo yake pamoja na miundombinu ya Kata hiyo.

Diwani Lucy aliwataka Wajumbe wake wa Kamati ya Siasa  kushirikiana kwa pamoja na Wananchi katika kuijenga Kata ya kisukuru iweze kuwa na Maendeleo .

Alisema changamoto za Kata hiyo atazitatua kwa kushirikiana Serikali  pamoja na Mbunge wa Segerea Bonah Kamoli Diwani Lucy aliwataka wananchi wake wenye Changamoto mbalimbali kuwasiliana na Ofisi yake kwa ajili ya kuzitatua .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here