Home LOCAL DIWANI FATUMA AELEZA MAFANIKIO YA KATA YA GEREZANI

DIWANI FATUMA AELEZA MAFANIKIO YA KATA YA GEREZANI

NA: HERI SHAABAN, (ILALA YETU)
DIWANI Fatuma Abubakari wa Kata ya Gerezani ameeleza mafaniko ya Kata ya Gerezani Wilayani Ilala katika sekta ya Elimu na uchumi .

Diwani Fatuma alisema hayo Dar es Salaam leo wakati wa kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani January hadi June 2021.



Fatuma alisema Kata ya Gerezani katika sekta Elimu imefanikiwa kuwa na shule za sekondari pamoja na shule za Msingi ambapo ina shule ya Sekondari Benjamini Mkapa,Sekondari Gerezani na Uhuru Mchanganyiko,kwa upande wa shule za Msingi Uhuru Mchanganyiko, Uhuru Wasichana.

Akielezea mafanikio ya Kata Gerezani kwa upande wa sekta ya uchumi , alisema kuna vikundi vya uzalishaji Mali Wanawake na Vijana zaidi ya 20 vikundi vya Ushirika .

“Katika Kata yangu nimefanya mambo makubwa sekta ya afya tuna zahanati ya Serikali ambayo inatoa huduma ndani ya Kata hii pamoja na Kata za jirani “ alisema Abubakari.


Diwani Fatuma alisema sekta Elimu amefanikiwa kujenga madarasa matatu
Gerezani shule ya Uhuru Wasichana na Uhuru Mchanganyiko ambapo ufaulu kwa shule za Msingi asilimia 96,idadi ya Wanafunzi walioongezeka asilimia 100 kwa uandikishaji.

Akielezea miradi aliyotekeleza ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na vyoo, sekondari Gerezani.

Aidha alisema mradi mwingine uliotekelezwa mahabara ya Fizikia Sekondari Gerezani vyoo matundu 12 shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko

Akielezea Idara ya Maendeleo ya Jamii wametoa mikopo kwa vikundi vya Kata hiyo na wanaendelea kutoa mikopo amewataka wananchi wake wafuate taratibu kwa kuunda vikundi na kusajili.

Akizungumzia Ulinzi na Usalama alisema uhalifu umeongezeka Kata ya Gerezani kutokana na ongezeko la Wamachinga katika maeneo si rasmi .

Wakati huohuo katika hatua nyingine kikao cha HALMASHAURI KUU KATA YA GEREZANI CCM kimeagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kimwamishe Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Gerezani Magharibi kwa kudaiwa makosa mbalimbali katika ufanyaji wa kazi zake kudaiwa kukosa uhadilifu na kushindwa kushirikiana na chama .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here