Home LOCAL DC ILALA ASOMA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI AKIELEZEA MAFANIKIO ILALA

DC ILALA ASOMA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI AKIELEZEA MAFANIKIO ILALA

NA: HERI SHAABAN.

MKUU wa Wilaya Ilala Arch Ng’wilabuzu Ludigija  amesoma  taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya January mpaka Juni katika Taarifa hiyo ilikuwa ikielezea mafanikio ndani ya Wilaya ya Ilala.

Akisoma taarifa hiyo Ludigija alisema Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM imetekeleza mradi wa Umeme wa REA Jimbo la Ukonga ,Mradi wa maji ya DAWASA sekta ya Elimu kwa kuongeza ufaulu na kujenga madarasa mapya 180. 

“Mafanikio katika Wilaya yangu ya Ilala mradi wa Umeme wa REA umefanikiwa kwa asilimia 90 ndani ya Jimbo la Ukonga maeneo ambayo hayajapata umeme huo kutokana na Changamoto mbalimbali nimeagiza nguzo 1000 zipelekwe kufanikisha mradi huo na wananchi wataunganishiwa umeme huo kwa shilingi 27,000/=” alisema Ludigija.

Ludigija akizungumzia Mradi wa maji wa DAWASA.alisema mradi wa DAWASA Ukonga maji yapo ya kutosha wananchi wote wa Jimbo la Ukonga watapa maji  katika mtandao huo.

Ludigija akizungumzia Sekta ya Elimu alisema kwa sasa ufaulu umeongezeka

vyumba 180 wamekamilisha vya madarasa na sekta ya Elimu mwaka 2022 Wilaya Ilala wamejipanga vizuri kwa ajili ya kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza .

Akizungumzia sekta ya Barabara bado changamoto hawana mtandao mzuri wa miundombinu hiyo ila Serikali imejipanga vizuri kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijni TARURA kuakikisha Barabara zote za Wananchi zinatengezwa.

Akizungumzia bonde la Mto Msimbazi madaraja yote ya Kisasa yamekamilika wananchi wanaanza kutumia madaraja hayo na kuunganisha mawasiliano ya Kinyerezi ,Ukonga, Gongolamboto ,Segerea mradi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa Kituo cha daladala Kinyerezi mwisho kinachojengwa na mradi wa kuboresha miundombinu .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here