Home BUSINESS BRELA YAHUDUMIA MAMIA YA WANANCHI MAONESHO YA MADINI GEITA

BRELA YAHUDUMIA MAMIA YA WANANCHI MAONESHO YA MADINI GEITA


Ofisa wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrend Andrew (mwenye miwani kushoto) akitoa Elimu kwa wadau waliotembelea Banda la BRELA katika maonesho ya Nne ya Teknolojia ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika uwanja wa kituo cha Uwekezaji, Bomba Mbili mkoani Geita.

Bw. Yusuph Nakapala  ( kushoto) akitoa elimu kwa wadau waliotembelea  banda la BRELA  katika maonesho  ya Nne ya  Teknolojia ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika uwanja wa kituo cha Uwekezaji,  Bomba Mbili mkoani Geita. Wadau hawa walipatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kurasimisha biashara pamoja na taratibu za Usajili wa Majina ya Biashara, Makampuni, Alama za Biashara na Huduma, utoaji wa Hataza, Leseni za Biashara kundi A na Leseni za Viwanda. Maonesho haya yaliyoanza Septemba 16,  2021  yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,   Mhe. Majaliwa Kassm Majaliwa  Septemba 22, 2021 na yatahitimishwa Septemba 26,2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here