Home BUSINESS BRELA YAENDESHA ZOEZI LA USAJILI NA KUTOA VYETI PAPO KWA PAPO JIJINI...

BRELA YAENDESHA ZOEZI LA USAJILI NA KUTOA VYETI PAPO KWA PAPO JIJINI MWANZA.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa (kulia) akimkabidhi Cheti cha usajili wa Jina la Biashara, Bw. Brighton Rugora (kushoto), baada ya usajili wa papo kwa papo katika banda la taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Biashara ya 16 ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Rock City Mall, jijini Mwanza. Maonesho haya yaliyoanza Agosti 28, 2021 yanatarajiwa kuhitimishwa Septemba 5, 2021. (PICHA NA: BRELA)

Maofisa wa Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA), wakitoa huduma kwa wateja waliofika kupata huduma mbalimbali katika banda la taasisi hiyo, kwenye Maonesho ya Biashara ya 16 ya Afrika Mashariki, yanayofanyika katika viwanja vya Rock City Mall, jijini Mwanza. Maofisa hao kutoka kushoto ni Bi. Angela Kimario, Bi. Winifrida Gaudence, Bi. Yvonne Maselle na Bw. Andrew Godfriend. (PICHA NA: BRELA)
Ofisa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Winifrida Gaudence akimkabidhi cheti cha Leseni ya Biashara kundi A Bw. Gilinde Kapula Fale, mara baada ya usajili wa papo kwa papo katika banda la taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Biashara ya 16 yanayoendelea katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza. Maonesho hayo yaliyoanza Agosti 28, 2021 na yanatarajiwa kuhitimishwa Septemba 5, 2021. (PICHA NA: BRELA)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here