Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akizungumza na Diwani wa Kata ya Kiwalani Mussa Kafana leo September 22/2021 katika ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo wengine Viongozu wa Chama (PICHA NA HERI SHAABAN).
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha kwanza Sekondari ya Kiwalani Wilayani Ilala leo September 22/2021 katika ziara ya Mbunge Bonah kukagua miradi ya Maendeleo (PICHA NA HERI SHAABAN).
NA: HERI SHAABAN
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Wilaya Ilala Bonah Ladslaus Kamoli, ameaidi fedha za jimbo shilingi milioni 30 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ikiwemo Sekta ya Elimu na Ulinzi na Usalama.
Mbunge Bonah alitoa ahadi ya kugawa fedha za mfuko wa Jimbo leo katika ziara yake ya kukagua miradi ya Maendeleo na kutatua kero za wananchi Kata za Kiwalani, Minazi Mirefu ,Vingunguti na TABATA ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na Wananchi, Walimu na Wanafunzi.
“Leo nimefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ndani ya Jimbo langu la Segerea katika baadhi ya Kata zenye changamoto nimezipatia fedha za Serikali ambazo zinazopitia mfuko wa Jimbo” alisema Bonah
Katika ziara hiyo Mbunge alisema fedha za Jimbo la Segerea shilingi milioni kumi zielekezwe kwa ajili ya Kituo cha kisasa cha Polisi Jamii Mwale Kata ya Minazi Mirefu kwa ajili ya masuala ya ulinzi na Usalama na kuagiza ifikapo January kiwe kimekamilika.
Pia Mbunge Bonah alisema fedha zingine shilingi milioni 20 sekta ya Elimu shule ya Msingi Mwale Kata ya Kiwalani kwa ajili ya elimu, awali shule hiyo waliomba milioni 35 Ofisi ya Mbunge imeelekeza shilingi milioni 20.
Aidha Mbunge Bonah aliwagiza Walimu Wakuu kujenga kwa kutumia (force akaunti)na kuitumia fedha za Serikali kwa malengo sahihi kwa kushirikiana na Diwani wa Kata husika
“Fedha hii ya Serikali naomba hapa niwe mkali zitafika kwa wakati itapitia akaunti za shule isitumike kinyume chake ” alisema.
Kwa upande wake Diwani wa Minazi Mirefu Godlisten Malisa alichangia shilingi laki 300,000/=kash kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Mwale kwa ajili ya Masuala ya Ulinzi na Usalama.
Diwani Godlisten Malisa alisema anaunga mkono juhudi za Mbunge Bonah katika juhudi zake za kuleta Maendeleo atashirikiana na Mbunge katika kila jambo ndani ya Kata Minazi Mirefu na kuunga mkono Juhudi za Serikali.
Mbunge Bonah ziara yake pia akizungumza na wananchi wa Bonde la Msimbazi Tabata Mangaribi na Vingunguti Wilaya ya Ilala.
Mwisho.