Home SPORTS BMT YAWAFUKUZA VIONGOZI WA MPIRA WA WAVU

BMT YAWAFUKUZA VIONGOZI WA MPIRA WA WAVU

Na; Stella KSTELLA KESSY

Baraza la michezo Taifa limewafukuza kazi viongozi wa mpira wa wavu Tanzania (TAVA)na hawataruhusiwa kabisa kujihusisha na masuala ya yoyote ya uongozi katika michezo nchini kwa miaka 2

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Neema Msitha alisema kuwa viongozi hao

mwenyekiti wa chama Cha mpira wa wavu Taifa Maj.Gen mstaafu Patric Mlowezi na Katibu wake Bw.Alfred Selengia wamehaibisha Taifa baada ya kushindwa kulipa ada ya mashindano na hotel ambayo walifikia ,Baraza la michezo la Taifa limechunguza kwa kina na kujiridhisha kuwa kulikuwa na uzembe ambao umehaibisha Taifa bila sababu za misingi.

” Na serikali imeingia gharama kubwa kurejesha wanamichezo hao nchini baada ya kuwa wamezuiwa nchini Rwanda ambapo walipewa nafasi ya kujieleza na kubaini kuwa licha ya serikali kupitia BMT ambayo ilitoa mchango wake kiasi Cha milioni 11.7 kwa kulipia gharama za ndege kwenda na kurudi.

Alifananua kuwa wakati serikali inatoa pesa hiyo wao walihaidi kuwa gharama nyingine watapata kwa wadhamini ambapo Baraza liliwashauri wabaki nchini na wao walilazimisha safari kwenda nje ya nchi wakiwa hawana hata pesa ya kulipa ada ya ushiriki.

Aliongeza Kuwa Kwa kufanya hivyo itakuwa fundisho kwa viongozi mbalimbali wanaosomamia michezo nchini kujua dhima yao Kwa jamii na Taifa,Baraza kwa mamlaka lilionayo lisheria chini ya Sheria Na.12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake Na 6 ya mwaka 1971 na kutumia kanuni za Baraza la michezo la Taifa 1999 fungu la 27 (3)linatoa adhabu hiyo.

Hata hivyo baraza limetoa onyo kali kwa makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Fredinard Mgeni na wajumbe wengine wa kamati ya utendaji kwa kutowajibika ipasavyo na wanawekwa chini ya uangalizi maalumu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here