Home SPORTS BIASHARA YAZIDI KUTAKATA KIMATAIFA.

BIASHARA YAZIDI KUTAKATA KIMATAIFA.

 

Na: Mwandishi wetu DAR ES SALAAM

BIASHARA United leo wametinga hatua ya awali katika mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dikhili FC katika Uwanja wa Azam Complex.

Katika dakika ya 19 Ramadhan Chombo  alifanikiwa kuipatia timu yake bao na dakika za 23 alifanikiwa kupata bao la pili.

Katika dakika ya 27 alikosa  penalti  ambayo ingemfanya aweze kusepa na mpira wake kwa kufunga hat trick.

Penalti hiyo Redondo alipiga kwa umakini ila iligonga mwamba na kufanya akwame kutimiza malengo yake ya kuweza kuipa bao la tatu timu yake ya Biashara United.

Katika mchezo wa kwanza ugenini Biashara United ilishinda kwa bao 1-0 hivyo jumla inasonga mbele kwa ushindi wa mabao 3-0.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here