Home BUSINESS BENKI YA NBC YAREJESHA TABASAMU KWA WATOTO.

BENKI YA NBC YAREJESHA TABASAMU KWA WATOTO.


Meneja wa NBC Tawi la Meru, Bi Florence Ng’wavi (wa tatu kulia) akiwa ameshika hundi ya mfano ya TSHs 22.5m kwenye picha ya pamoja na Mkuu Taasisi ya Same Qualities, Dk Peter Mabula (wa pili kushoto) baada ya kukamilika kwa mbio za nyika zilizoandaliwa na taasisi hiyo. Benki hiyo imetoa msaada wa kiasi hicho hicho cha fedha kugharamia matibabu na upasuaji watoto 30 wenye tatizo la mdomo sungura katika mikoa mbali mbali nchini. Wengine katika picha ni Mameneja Mauzo wa NBC, Bi Belinda Chelese (kulia) na Neema Soka (kushoto) pamoja na Gerald Babu (mwenye kofia) ambaye Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Arusha.


Meneja wa NBC Tawi la Meru, Bi Florence Ng’wavi (wa nne kulia) akishikana mikono na Nd John Bayo (wa pili kushoto) wakati akimkabidhi hundi ya mfano ya TSHs 22.5m baada ya benki hiyo kutoa msaada wa kiasi hicho hicho cha fedha kwa Taasisi ya Same Qualities iliyo chini ya Dk Peter Mabula (wa pili kulia) baada ya kukamilika kwa mbio za nyika zilizoandaliwa na taasisi hiyo Jijini Arusha. Kiasi hicho cha fedha kitaenda kugharamia matibabu na upasuaji wa watoto 30 wenye tatizo la mdomo sungura katika mikoa mbali mbali nchini. Wengine katika picha ni Mameneja Mauzo wa NBC, Bi Belinda Chelese (wa nne kushoto) na Neema Soka (wa tatu kushoto) pamoja na maofisa wengine wa Benki ya Taifa ya Biashara.

ARUSHA.

Benki ya Taifa ya Biashara imejipambanua tena kuwa ni taasisi inayojali jamii kwa kurejesha kiasi kidogo cha faida kwa dhumuni la kufadhili programu na miradi mbali mbali nchini. Hii ni kutokana sera ya benki hiyo ya kurejesha kwa jamii sehemu ya faida inayopata kutokana na kuwahudumia Watanzania. Sera ambayo imesimamia nguzo kuu tatu za afya, elimu na ustawi wa jamii.

 

Hayo yamebainika Jijini Arusha katika mbio za nyika zilizoratibiwa na kuandaliwa na Taasisi ya Same Qualities iliyojikita katika kutoa huduma za upasuaji bure kwa watoto wenye tatizo la mdomo wazi au mdomo sungura kama inavyojulikana na wengi. Mbio hizo zilizoanza na kuishia katika uwanja wa Amri Abeid Karume na kuhuduriwa na wadau mbali mbali kama Benki ya NBC ikiwa mdamini mkuu, Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha, Jeshi la Polisi Usalama Barabarani na Taasisi ya Smile Train zikiwa na dhumuni la kuongeza ufahamu na uelewa wa tatizo la mdomo sungura.

 

Zaidi ya Benki ya NBC na wafanyakazi wake wa Tawi la Meru kushiriki katika mbio hizo, benki hiyo ilitoa kiasi cha TSHs 22,500,000 itakayoenda kugharamia upasuaji wa watoto takriban 30 ili kuwarejeshea tabasamu zao. Huduma za upasuaji zitafanyika katika kambi maalum za matibabu zilizoratibiwa na Taasisi ya Same Qualities katika mikoa ya Tabora, Moshi na Shinyanga kabla ya mwisho wa mwaka huu.

 

Akizungumza baada ya kukamilisha mbio za kilomita 10, Meneja wa Tawi la NBC Meru Bi Florence Ng’wavi alisema kurejesha katika jamii ni tamaduni ya benki hiyo kongwe yenye zaidi ya miaka 50 nchini, tamaduni ambayo benki hiyo itaendeleza kwa miaka ijayo ili kugusa maeneo mengi zaidi. 

 

“Lengo letu katika kutoa msaada huu kwanza ni kurejesha tabasamu kwa watoto hawa pamoja na familia zao lakini pia ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kufikisha huduma mbali mbali kwenye jamii za Kitanzanoa zenye uhitaji.” Alisema Bi Florence.

 

Kwa upande wake, mratibu na wa kambi hizo za matibabu na Mkuu wa Taasisi ya Same Qualities, Dokta Peter Mabula alishukuru uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara kwa msaada huo lakini pia alitoa wito kwa benki hiyo kuendelea kushirikiana na taasisi yake katika kuratibu na kudhamini kambi za matibabu zitakazofanyika mbeleni.

 

Aidha Dk Mabula aliimwagia sifa benki hiyo kwa kuwafuata ofisini kwao na kufanikisha kwa ufanisi mkubwa taasisi yake kufungua NBC Jamii Account pamoja na kupatikana kwa fedha za udhamini kwa haraka. “Tulivyoomba tulipata ushirikiano wa hali ya juu na walitusaidia sana kuhakikisha fedha imengia katika akaunti zetu nasi tutahakikisha zitatumika kama ilivyokusudiwa.” Aliseka Dk Mabula. 

 

Akiongelea NBC Jamii Account, Meneja wa Mauzo wa Benki ya NBC Tawi la Meru, Bi Belinda Chelese alisema kwamba akaunti hiyo ni maalum kwa asasi au taasisi zisizo za kiserikali zikiwemo za kijamii na kidini zinazojiendesha bila faida kwa lengo la kuhudumia jamii. Aidha Bi Belinda Chelese alisema kuwa akaunti hiyo ina masharti nafuu ya kufungua na haina makato ya uendeshaji ya kila na kusihi taasisi zingine kufungua NBC Jamii Akaunti katika matawi ya benki hiyo nchini.

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here