Home SPORTS AZAM FC YAENDELEZA UBABE SHIRIKISHO

AZAM FC YAENDELEZA UBABE SHIRIKISHO


MWANDISHI WETU.

KIKOSI cha  Azam FC kimefanikiwa kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Horseed ya Somalia jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la Azam FC katika mchezo huo wa marudiano Raundi ya Awali limefungwa na kiungo Ismail Aziz Kada dakika ya 38 na kwa matokeo hayo wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla 4-1.

Ambapo katika mchezo wa kwanza  Horseed 3-1 kwenye mechi ya kwanza hapo hapo Chamazi Jumamosi iliyopita na sasa itakutana na Pyramids ya Misri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here