Home Uncategorized ZIARA YA RC HAPI HAIJAMUACHA SALAMA MHANDISI HALMASHAURI YA TARIME

ZIARA YA RC HAPI HAIJAMUACHA SALAMA MHANDISI HALMASHAURI YA TARIME

Mhandisi Ernest Maungo(Kushoto aliyeweka miwani kichwani) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi wakati akikagua Jengo la Bwalo la Sekondari ya Manga, ikiwa sehemu ya ziara yake wilayani Tarime Leo.

Na: Mwandishi Wetu,TARIME.

MHANDISI wa Halmashauri ya Tarime, Eng. Ernest Maungo Leo amewekwa  rumande na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime, baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi kubaini madudu kwenye Mradi wa Ujenzi wa Bwalo la Shule ya Sekondari ya Manga iliyopo Kijiji cha Surubu Kata ya Komaso.

Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Editha Nakei amesema gharama ya mradi huo ni zaidi ya Sh milioni 100  na kwamba mpaka ulipofikia umetumia Sh milioni 96.4.

Hata hivyo RC Hapi baada ya kushuhudia jinsi nguzo za jengo hilo zilivyopinda na kuta zake kuinama, ameamuru livunjwe haraka ili kuepusha hatari  inayoweza kutokea endapo litaanguka.

Pia ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kukamata na kuhoji kila aliyehusika na mradi huo, ili atakayethibitika kuhusika na ‘kutupa jalalani‘ fedha hizo za serikali azirudishe.

Bodi ya Shule hiyo pia imevunjwa na Mkuu wa Mkoa Hapi ambaye ametaka kila mjumbe ahojiwe na TAKUKURU na kwamba anaweza kuamua vinginevyo baada ya uchunguzi kukamilika.

Akizungimza nasi katika mahojiano maalumu, Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Mara, Hassan Mossi hakukanusha wala kukiri kuagiza kukamatwa Eng. Maungo, ingawa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime, RPC William Mkonda amethibitisha kuwa wanaye.

Mkuu Mossi amesema baadhi ya miradi ukiwemo wa Jengo hilo walishaanza kuifanyia kazi na uchunguzi upo kwenye hatua ambazo siyo sahihi kwao kuzizungumzia kwenye vyombo vya habari.

“Wakati wa kutoa taarifa kwa umma ukiwadia, tutafanya hivyo nina hakika mnafahamu kuwa hii ni taasisi ya uchunguzi,”amesema Mossi.

Naye Afisa Elimu – Sekondari wa Halmashauri hiyo, Victor Emmanuel akizungumza nadi katika mahojiano maalumu amesema endapo ujenzi huo ungekamilika jengo lingehudumia watu 400.

Previous articleDITOPILE AWAVAA WANASIASA NA VIONGOZI WA DINI WANAOPOTOSHA KUHUSU CHANJO
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI HII YA LEO IJUMAA AGOSTI 13-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here