Home BUSINESS ZAO LA DENGU LATELEKEZWA SHAMBANI KISA DHAHABU

ZAO LA DENGU LATELEKEZWA SHAMBANI KISA DHAHABU

Shamba lenye dengu iliyotelekezwa na kuwekewa viroba vya mawe yanayosadikiwa kuwa na dhahabu.

Mmiliki wa Shamba Bwa. Hamisi Lukubanja akionyesha Shamba lake lenye dengu iliyo tayari kwa kuvunwa.

Na: Saimon Mghendi, SHINYANGA.

Katika hali isiyokua ya kawaida Wanakijiji cha Nyandolwa katika kata ya Mwenge, Wilaya ya  shinyanga Vijijini, Mkoani Shinyanga, Wametelekeza mazao aina ya dengu na kuamia kwenye uchimbaji wa dhahabu Licha ya kwamba Mazao hayo yamefikia wakati wa kuvunwa.

Hali hiyo inatokana na kuibuka kwa machimbo mapya katika Kijiji hicho, jambo liliopelekea wakulima hao kuachana na uvunaji wa zao la dengu na kuamia kwenye dhahabu ambapo wanapata kipato Zaidi.

Akifafanua mbele ya Waandishi wa Habari waliofika katika machimbo ya Nyandolwa jana Kujionea hali halisi ilivyo, Hamisi Lukubanija, Mkulima wadengu lakini pia ni mliliki wa mashamba ambayo yanachimbwa dhahabu, alisema kuwa hawezi akang’ang’ana  na dengu wakati anapata fedha nyingi kutokana shamba lake kuchimbwa kwa Dhahabu.

“Maeneo haya ndipo ninapolima dengu na mpunga lakini kumetokea neema ya dhahabu kwahiyo mimi na watu hawa tumekubaliana wachimbe tu dhahabu kwani ukiweka viroba vya mawe ya dhahabu kwenye dengu na kiroba kimoja kina thamani ya Tsh. Laki mbili  kuna ubaya gani?” Alihoji Lukubanija.

Hata hivyo baadhi ya wana Kijiji wa Nyandolwa walilalamikia juu ya kukosa watu wa kuvuna Mazao yao aina ya dengu wakieleza sababu kubwa ni kuwepo kwa machimbo ya dhahabu katika eneo hilo ambapo wamedai watu hao hupata fedha nyingi kwenye machimbo kuliko wakivuna dengu.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here