NA: MWANDISHI WETU.
VIJANA wazalendo wa mkoa wa Morogoro wakishirikiana kwa pamoja wameandaa siku maalim ya kutembelea moja ya kituo cha kulelea watoto wanaoishi mazingira magum katika mkoa huo.
Akizungumz na ukurasa wa huu katibu wa vijana hao Fareed Mohammed, amesema watarajia kutembelea kituo kiitwachwa kwa lengo la kutembelea na kupeleka baadhi ya mahitaji.
“Sisi kama vijana tumeungana kutembelea kituo cha Erick Memorial Foundation, tuta tumia siku nzima kwa kucheza, kula na kutoa ushauri mbalimbali kwa watoto hao ambao wanahitaji uangalizi wa juu kutoka kwa jamii yetu,” Fareed Mohammed.
Aliongeza kuwa wanahitaji mchele, maharage, Ngano, Unga wa ugali, Mafuta ya kupikia, Nguo, Sabuni, Dawa za mswaki na vifaa vya shuleni wanakaribisha wadau mbalimbali pamoja na wanchi kuungana nao ili kufanikisha siku hiyo.
“Tunaomba makampuni, taasisi na wanachi ambao wana wiwa kuungana nasi wakaribie ili tuweze kuungana ambaye anaweza kuleta baadhi ya mahitaji anaweza kutuleta katika hoteli ya Oasisi atakabidhi mapokezi mzigo huo utakuwa umetufikia.”