DAR ES SALAAM
KLABU ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo Agosti 26 imetangza rasimi App yao itakayowawezesha mashabiki na wapenzi wao kupata taarifa mbalimbali za timu yao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi huo Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wameanzisha APP hiyo kwa ajili ya kusogeza taarifa mbalimbali za klabu hiyo.
“Kupitia App ya Simba tutawafikia mashabiki wote wa Simba,hivyo hapo mbeleni hata wanaotumia tochi watapata taarifa.Kila mwana Simba akilipa sh.2000 tu simba itakuwa na fedha kiasi gani? Watakuwa na uwezo wa kununua wachezaji wa Simba na kubwa zaidi wana Simba watapata kila kinachohusu klabu yao tena kwa wakati sahihi,”amesema Kamwaga.
Amefafanua zaidi Simba imeamua kuzindua App yake na hayo ni mapinduzi makubwa ya kidigitali. “Kwa sasa dunia iko kwenye zama za taarifa na katika zama zenye taarifa Simba inakuwa klabu ya kwanza Tanzania kwenda kwenye dunia ambako iko.
“Simba App ni jukwaa la kidigitali ambalo wana Simba watakuwa wakipata taarifa sahihi na wakati unaofaa,lakini sio tu kupata taarifa tu tutakwenda kuingiza fedha kupitia fedha.ambayo itatokana na wana Simba kujiunga kwa kujisajili.
“Kuanzia leo hii tutaanza kutoa taarifa za Simba, hata Simba Day tutaitangaza kupitia kwenye Simba App.Leo timu yetu inacheza kule Moroccp na timu ya daraja la kwanza,hivyo kupitia Simba App majina ya wachezaji na kila kinachoendelea kitawekwa humo,”amesema.
Kwa upande wake Mtaalam aliyetengeneza Simba App Given Edward kutoka My Elimu amesema kabla ya kuzinduliwa kwa App hiyo wamefanya utafiti na kujiridhisha kuwa huu ni wakati sahihi kutokana na ukubwa wa Simba.
“Jambo moja ya kwenda na Simba App ni kwasababu Simba ni kubwa, ina mashabiki mamilioni kwa mamilioni.Simba ina mashabiki zaidi ya wale milioni 60 wanaoingia uwanjani.