Home LOCAL TCU YAFUNGUA AWAMU YA PILI YA UDAHILI 2021/2022, YAONYA WANAFUNZI KUTOTUMIA VISHOKA.

TCU YAFUNGUA AWAMU YA PILI YA UDAHILI 2021/2022, YAONYA WANAFUNZI KUTOTUMIA VISHOKA.


Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) katika mkutano wake uliofanyika kwenye Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 23,2021. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) Jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Mkurugenzi wa uratibu wa Udahili na utunzaji wa Kanzidata wa Time hiyo Dkt Kokuberwa Kulunzi-mollel katika mkutano wake uliofanyika kwenye Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
 
Mkurugenzi wa uratibu wa Udahili na utunzaji wa Kanzidata wa Time hiyo Dkt Kokuberwa Kulunzi-mollel (kushoto aliyekaa) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (TCU) Jorlin Kagaruki (kulia) muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, Dar es Salaam.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa Awamu ya pili ya udahili wa Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2021/2022 kuanzia Agosti 24 hadi Septemba 6, 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Profesa Charles Kihampa amesema kuwa Dirisha hilo limefunguliwa ili kuendelea kutoa nafasi kwa wananfunzi wenye sifa kujiunga na Elimu ya Juu na kusisitiza kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakudahiliwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali kuitumia  fursa hiyo vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.

Aidha Profesa Kihampa ameendelea kuwakumbusha waombaji wote wa udahili wa Shahada ya kwanza kuwa masuala yote yanayohusiana na udahili au kujithibitisha kwenye Chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

“Waombaji udahili wa Shahada ya kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika Chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika na kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa” Amese,a Prof. Kihampa.

Pia Profesa Kihampa amesema kuwa TCU inawaasa wananchi wote kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri na kudai kutoa huduma ya kusaidia jinsi ya kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini. 

Awali akitoa taafa ya yake ya udahili wa Awamu ya kwanza amesema kuwa jumla ya waombaji 92,809 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 74 vilivyoidhinishwa kudahili nakwamba jumla ya programu 724 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 686 mwaka 2020/2021.

“Pia katika Awamu ya kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 68,019 sawa na asilimia 73.2 ya waombaji wote waliioomba udahili wameshapata udahili vyuoni” ameongeza Prof. Kihampa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here