Home LOCAL TATIZO LA MAJI BUTIAMA KUTATULIWA SEPTEMBA MWAKA HUU

TATIZO LA MAJI BUTIAMA KUTATULIWA SEPTEMBA MWAKA HUU

Picha Na: Maktaba.

Na: Mwandishi wetu, BUTIAMA.

WILAYA ya Butiama mkoani Mara haina huduma za maji kwa Miezi Miwili sasa kufuatia pampu ya kusukumia maji kufa.

Mkuu wa Mkoa (RC) huo, Ally Hapi alisema licha ya jitihada za kutatua tatizo hilo kufanyika, tatizo hilo litaendelea kuwapo mpaka Septemba Mwaka huu.

“Tulitafuta pampu mbadala mkoa mzima tukakosa hata kwenye mikoa ya jirani hatukufanikiwa kupata hata ya kuazimwa, kwa sasa serikali imetoa fedha ili inunuliwe mpya na kufungwa,” alisema.

Aliomba radhi kwa wananchi wa Wilaya hiyo, akisema anafahamu wanapata adha nyingi kutokana na changamoto hiyo.

Alisema pamoja na ununuzi wa pampu hiyo, upo mradi mkubwa wa kuboresha huduma za maji utakaohudumia vijiji 18 wilaya humo ambao wamekubaliana mpaka kufikia Disemba mwaka ujao uwe umekamilika.

Miwsho.

Previous articleRAIS SAMIA AWEKA HADHARANI MKEKA WA WAKURUGENZI
Next articleCHUO KIKUU CHA SUA CHAVUKA LENGO LA UDAHILI KWA WANAFUNZI KOZI YA NYUKI NA ASALI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here