Home ENTERTAINMENTS TAREHE YA KUFANYIKA KWA TAMASHA LA SHUKURANI YABADILIKA, SASA NI OKTOBA 31,2021

TAREHE YA KUFANYIKA KWA TAMASHA LA SHUKURANI YABADILIKA, SASA NI OKTOBA 31,2021


Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Shukurani akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam wakati akitangaza mabadiliko ya tarehe ya kufanyika kwa tamasha hilo ambalo sasa litafanyika Oktoba 31 badala ya Oktoba 3, 2021. 

Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Shukurani akimsikiliza mwimbaji wa nyimbo za injili Edson Mwasabwite wakati akizungumza katika mkutano huo uliofanyika ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam wakati akitangaza mabadiliko ya tarehe ya kufanyika kwa tamasha hilo ambalo sasa litafanyika Oktoba 31 badala ya Oktoba 3, 2021.

DAR ES SALAAM.

MUANDAAJI wa Tamasha la Shukurani, kutoka kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama’ametangaza mabadiliko ya tamasha hilo na kutaja tarehe rasmi ya tamasha hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa kilicho badilika ni tarehe ambayo tamasha hivyo itafanyika tarehe
Octoba 30 mwaka huu na sio Octoba 3 kama ambavyo alikuwa amesema awali.

“Mashabiki wakae mkao wa kula kwani tumejipanga vizuri na wasanii mbalimbali wakubwa wataimba live,” alisema Msama.

Pia waandaaji wa tamasha hilo Msama Promotion wameahidi kufanya tamasha la kihistoria, kutakuwa na wasanii mbalimbali akiwemo Upendo Nkone na wengine wengi.

Hata hivyo Msama ameeleza kuwa tamasha hilo lipo kwa ajili ya kusifu na kuabudu huku burudani ikiwa ni sehemu ya kuwaeka karibu watu wa Mungu kutoka sehemu mbalimbali nje na ndani ya Mji wa Dar es salaam kwani tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Credit – Fullshangwe Blog

 

Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.NNE AGOSTI 31-2021
Next articleMATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA BUNGE LEO AGOSTI 31,2021 JIJINI DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here