Home BUSINESS TANZANIA KINARA UWEKEZAJI AFRIKA MASHARIKI

TANZANIA KINARA UWEKEZAJI AFRIKA MASHARIKI


Na: Beatrice Sanga- MAELEZO.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimebainisha kwamba Tanzania imepata kiwango kikubwa cha uwekezaji kinachofikia dola za Kimarekani bilioni 1.0 ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa mwaka 2020, ambapo katika ukanda wa  Afrika Mashariki, Burundi ina uwekezaji wa ($6Milioni), Kenya ($717Milioni), Rwanda ($135Milioni), na Uganda ($823Milioni)na kuifanya Tanzania kuwa kinara kwa ukanda huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi  wa TIC, Maduhu Kazi amesema takwimu hizo ni za kiwango cha uwekezaji duniani mwaka jana kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Biashara Sawia Kimataifa la (UNCTAD)

“Tanzania imepata uwekezaji mkubwa ukilinganisha na nchi nyingine za EAC. Changamoto ya UVIKO-19 imesababisha Tanzania kuvutia mitaji ya viwanda vya madawa ya Binadamu,”amesema Maduhu.

Alisema katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 idadi ya miradi ya uwekezaji ya watanzania pekee iliyosajiliwa ni ni 66 sawa na asilimia 28 ya miradi yote iliyosajiliwa kwa kipindi hicho na kupelekea ajira nyingi kwa watanzania.

Ameongeza kuwa, katika kipindi cha mwaka 2020/21 TIC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imetekeleza majukumu yake ipasavyo hivyo kupelekea maboresho yaliyosababisha kukua kwa uwekezaji nchini.

Amesema kuwa Miongoni mwa maboresho yaliyofanyika ni Uboreshaji wa Huduma za Mahala Pamoja, Mfumo wa Pamoja wa Huduma kwa Wawekezaji Tanzania, Utoaji wa Vyeti vya Vivutio, Mfumo wa OSS- External Portal, Kuanzishwa kwa Call Centre na Kuhamasisha Uwekezaji wa Viwanda na Kuboresha Upatikanaji wa Ardhi.

“TIC imetenga ardhi inayofaa kwa ajili ya uwekezaji wa aina hiyo ambapo kanzidata ya Ardhi ya Kituo kwa mwaka 2020/21 imesajili maeneo 273 yenye ukubwa wa Hekta 159, 720 chini ya Taasisi za Serikali na Halmashauri na maeneo 23 yenye ukubwa wa hekta 9240 kutoka kwa Watanzania binafsi, “amesema Maduhu.

 Pia kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Binafsi (Blue Print) amesema hadi kufikia Desemba 2020 Serikali ilikuwa imetunga na kurekebisha sheria mbalimbali, kuweka mifumo ya Elektroniki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here