Home Uncategorized STAMICO, BUCKREEF WASAINI MKATABA WA UCHORONGAJI WA THAMANI YA SH. BILION 4.

STAMICO, BUCKREEF WASAINI MKATABA WA UCHORONGAJI WA THAMANI YA SH. BILION 4.

Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Dk. Venance Mwasse (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Buckreef, Khalaf Rashid wakionesha mkataba huo mara baada ya kuusaini katikati ni Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dk. Venance Mwasse (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Buckreef, Khalaf Rashid(wa kwanza kulia) wakisaini mktaba wa uchorongaji wenye thamani ya SH bilioni nne. Katikati ni Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila akishuhudia.

NA: MWANDISHI WETU.

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesaini mkataba wa uchorongaji na Mgodi wa Madini wa Buckreef (Buckreef Gold Company Ltd) ambayo ni kampuni inayochimba madini katika mkoa wa Geita.

Mkataba huo wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni nne, utadumu kwa muda wa mwaka mmoja.

Akizungumza katika hafla ya kusaini kandarasi hiyo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dk. Venance Mwasse alisema mkataba huo utahusisha mitambo ya kisasa ya STAMICO ya uchorongaji ya Diamond Drilling (DD) na Reverse Circulation (RC).

Alisema jukumu hilo la uchorongaji ni ya mwazo na utahusisha uchorongaji wa mita 10,000 za awali.

Alisema mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka huu wa fedha 2021.

“STAMICO linamiliki mitambo mipya mitatu ya kisasa ya uchorongaji yenye uwezo wa kutoa huduma ya uchorongaji kwa wateja wake kwa haraka zaidi na kwa viwango vya juu zaidi kiushindani.

“Kufuatia utiaji saini wa mkataba huo na kuanza kazi Shirika linatarajiwa kutoa ajira za muda mfupi kwa wakazi wazawa na kuchangia uchumi wa wilaya ya Geita na taifa kwa ujumla,” alisema. 

Alisema shirika linatoa wito kwa wachimbaji wadogo kujikita katika uchimbaji wa kisasa unaozingatia usalama migodini na utunzaji wa mazingira.

“Tunaipogeza Kampuni ya Buckreef kupitia Mkurugezi Khalaf Rashid kwa kuiamini STAMICO kufanya kazi hii ya uchorongaji. “Shirika linaahidi kufanya kazi kwa bidii na uweledi mkubwa ili kutoa matokea yenye tija kwa kuwa ina mitambo ya kisasa na wataalamu wa kutosha.

“Shirika linatoa wito kwa wamiliki wa migodi na makampuni mengine nchini kutumia mitambo ya kisasa ya uchorongaji kutoka Shirika la madini la Taifa, kwani lina uwezo, wataalamu na vifaa vya kufanya kazi ya uchorogaji,” alisema. 

Aidha, Mkurugenzi wa Kampuni ya Buckreef, Khalaf Rashid aliishukuru Stamico kwa kuendelea kushirikiana pamoja katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika kuinua sekta ya madini nchini.

Wakati mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjilwa mbali na kuipongeza Stamico kwa miradi mbalimbali ya kimkakati iliyofanikiwa kuitekeleza, pia alilitaka Shirika hilo kuendelea kujiimarisha na kumiliki mgodi wake binafsi kwa asilimia 100.

Alisema mkataba huo uchorongaji ni mwendelezo wa kazi nzuri zinazofanywa na STamico kwani mwaka jana Stamico ilipata zabuni ya kuchoronga na kutafiti madini kutoka kampuni ya madini ya Geita Gold Mine Ltd. (GGML) wenye thamani ya Sh bilioni tisa.
“Ubora wa kazi zenu ndio unawafanya muendelee kupata zabuni nyingine kubwa na nzuri, Serikali tutaendelea kuwaunga mkono kwa sababu hata sasa utegemezi wa Stamico kwa serikali ni mdogo.

“Tutaendelea kuwaunga mkono hadi utegemezi uishe lakini pia kuhakikisha shirika linaendelea kutoa gawio kwa serikali kama mlivyoanza mwaka huu

“Shirika lilikuwa limekufa na lilitaka kufutwa kabisa lakini katika uongozi wa sasa ndani ya kipindi cha miaka mine mmefanikiwa kulifufua,” alisema.
MWISHO

 

 

 

Previous articleMAJALIWA: SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.NNE AGOSTI 31-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here